SAYARI YA MIDUARA
KWA AJILI YA DUNIA= KWA AJILI YETU
Mradi wa “sayari ya miduara” ni mradi wa hiari wa kimataifa ambao una lengo la kuunganisha watu, sayari na ‘nafsi yake’. Uhusiano huu hutokana, huendelea na kukua pamoja na mti ambao umepandwa ndani ya mradi huu. Watu huunganishwa na Sayari kwa kupanda miti katika mviringo wa ukubwa wa mita 20. Ni zoezi la kijamii kwa kuwa linafanya watu wajumuike pamoja. Uunganisho wa mizizi unaashiria muungano kati ya watu.
KWA AJILI YA MITI
Mojawapo ya malengo ya mradi wetu ni kuokoa mimea changa ambayo inapatikana mahala pasipofaa kwaukuaji wao kisha kuipanda tena kwingineko.
KWA AJILI YA MAENEO
Changamoto kuu ya mradi huu ni kupata mahala mwafaka pa upanzi. Tungependa kupanda miti kwenye maeneo ya umma yasiyo na matokeo bora kiuchumi na yanayohitaji utunzi na urekebishaji.Tunahitaji kuwasiliana na manispaa na mashamba ya serikali ili kupata maeneo madogo madogo yanayohitaji urekebishaji. Moja ya malengo ya mradi huu ni kutunza maeneo yaliyotelekezwa, yalizofanywa mahame nayaliyoharibika. Maeneo haya yanahitaji kulimwa upya ili yawe na nafasi za ukuzaji na uunganishi.
KWA JAMII ZINAZOKUSUDIWA/MASHINANI
Mradi wa’ Sayari ya miduara’ uatoa fursa ya kutengeneza mahusiano mapya baina ya watu, kufufua maeneo na sayari. Mmradi huu unaweza kutumika kusaidia juhudi za mtaani na kutumika kama msingi wa kukuza uhusiano kati ya watu.
KWA AJILI YA MAMA
Mradi huu unasaidia kukuza uhusiano mitaani na kudumisha ustawi endelevu wa mazingira ya kijamii na piaushirikiano bora kati ya binadamu na sayari.
Circles from Kenya
KWA AJILI YA ULIMWENGU MZIMA
Mduara huu unaweza kutazamwa kama ishara ya ushirikiano, ukamilifu na udaima.
KWA AJILI YETU (TENA)
Tunaamini kuwa, kwa binadamu, mduara huu utaleta hitaji kamilifu la mahusiano ya kina na asili, na shughuli yenye maana iliyotekelezwa kwa ajili ya jamii na ubinadamu.
Kiungo cha ukurasa wa wavuti: https://planetofcircles.earth/?lang=en